Wafaransa waandaa maonyesho ya mapishi Tanzania

Thursday March 14 2019

 

By Kelvin Matandiko Mwananchi [email protected]

Dar es salaam. Umewahi kula chakula cha Kifaransa au kushiriki burudani ya muziki wa Kifaransa?

Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam wameandaa maonyesho ya mapishi ya vyakula vya Kifaransa yatakayofanyika Machi 21, 2019.

Maonyesho hayo yatahusisha watu wa kutoka mataifa mbalimbali waishio hapa nchini.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier amewaambia wanahabari leo Alhamisi Machi 14 ,2019 kwamba sababu za kufanyika tukio hilo ni kutangaza utamaduni wa taifa hilo kwa njia ya vyakula na burudani ya muziki.

"Kwa mara ya kwanza inafanyika hapa nchini na Watanzania wote wanakaribishwa, chakula unalipia lakini baada ya chakula kutakuwa na muziki wa bila kiingilio,’’ amesema Balozi Clavier.

Advertisement