Wahitimu elimu ya juu ya uhasibu watangaziwa ajira

Saturday September 29 2018Mkurugenzi Mtendaji  wa NBAA,  Pius Maneno.

Mkurugenzi Mtendaji  wa NBAA,  Pius Maneno. 

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) imetangaza neema kwa wahitimu wa elimu ya juu ya uhasibu (CPA)  nchini wa mwaka  2018 wasio na ajira hadi sasa.

Leo Septemba 29, 2018  katika mahafali ya 40 ya bodi hiyo Mkurugenzi Mtendaji  wa NBAA,  Pius Maneno amesema wote ambao hawana ajira kuripoti katika ofisi za bodi hiyo Jumatatu Oktoba Mosi, 2018  katika idara ya utaalamu na huduma za ushauri.

"CPA wa mwaka huu ambaye hana ajira akaripoti Jumatatu ofisi za NBAA," amesema Maneno.

Baada ya kutamka kauli hiyo watu waliokuwepo katika mahafali hayo wameshangilia kwa takribani dakika moja.

Mahafali hayo yamehusisha wahitimu 714 katika kozi mbalimbali, wakiwemo wa CPA.

 

Advertisement