Wakazi Mbeya wajitokeza kwa wingi kumsikiliza Magufuli

Friday April 26 2019

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya waliyojitokeza uwanja wa Ruanda Nzovwe kwa ajili ya kumsikiliza Rais Magufuri ambaye anatarajia kuhutubia muda mfupi ujao.Picha na Ipyana Samson. 

By Ipyana Samson, Mwananchi [email protected]

Mbeya. Wananchi wa jiji la Mbeya kutoka maeneo tofauti wameanza kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Ruanda Nzovwe ambako Rais  John Magufuli atazungumza na wakazi wa jiji hili.

Mcl digital imefika viwanja hivyo na kushuhudia wananchi wakijitokeza kwa makundi huku wengine wakiingia kwa kuimba nyimbo za kumkaribisha Rais Magufuli.

Hata hivyo kila mwananchi anayefika uwanjani hapa kwa ajili ya kumsikiliza kiongozi huyo wa nchi lazima akaguliwe na vikosi vya ulinzi na usalama.

 

Rais Magufuli anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa jiji la Mbeya kuanzia saa sita mchana.

Aidha muda huu shughuli zinazoendelea uwanjani hapa ni burudani kutoka vikundi mbalimbali vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuburudisha wananchi watakaojitokeza uwanjani hapo.

Advertisement