Waliofariki ajali ya lori la mafuta Morogoro wafikia 85

Muktasari:

  • Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya moto wa lori la mafura ya petroli iliyotokea eneo la Msamvu Morogoro, imefika 85 baada ya majeruhi watatu kufariki leo jioni Jumatano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili

Morogoro. Majeruhi watatu kati ya 32 waliokuwa wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam nchini Tanzania wamefariki dunia.

Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Kebwe amesema majeruhi hao wamefariki leo jioni Jumatano Agosti 14, 2019 hivyo kufikia idadi ya waliofariki kufikia 85.

Mkuu huyo wa mkoa amesema majeruhi 16 waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro wanaendelea vyema huku akiwaomba ndugu kujitokeza kuwajulia hali majeruhi hao pamoja na wale waliopo Muhimbili.

Awali, leo asubuhi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha akitoa taarifa za majeruhi hao alisema walikuwa wamebakia 32 baada ya sita kufariki usiku wa kuamkia leo.

Alisema kati ya majeruhi hao 17 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine 15 wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya Sewahaji.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi