Wanaoshambulia kanisa ni shetani

Muktasari:

Leo kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa na viongozi wa kanisa hilo wanaotoka zaidi ya nchi 130 ulimwenguni

Rome, Italia. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema wale wanaolishambulia kanisa wanajihusisha na shetani.

Kauli hiyo ameitoa jana Februari 20 mbele ya mahujaji na kusema kuwa kasoro katika kanisa lazima zikemewe kwa lengo la kulisahihisha kanisa.

Lakini amesema wanaofanya hivyo bila ya kuwa na upendo na wanatumia muda wao kulishutumu kanisa, ni marafiki au ndugu wa shetani.

Papa Francis ameyazungumza hayo siku moja kabla ya leo kufanyika mkutano wa kilele wa maaskofu kuhusu jinsi ya kukabiliana na visa vya unyanyasaji wa kingono unaofanywa na makasisi na namna ya kuwalinda watoto na waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.

Wakosoaji, akiwemo balozi wa zamani wa Vatican nchini Marekani, wamemshutumu Papa kwa kushindwa kukabiliana ipasavyo na viongozi wa juu wa kanisa Katoliki pamoja na mapadri ambao wanatuhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono.