VIDEO: Wastaafu 10,500 wa PSSSF hawajahakikiwa

Meneja kiongozi uhusiano na elimu kwa umma wa mfuko huo, Eunice Chiume 

Muktasari:

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema wastaafu 10,500 kati ya 124,500 hawajahakikiwa katika daftari la wastaafu la mfuko huo


Dar es Salaam. Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema wastaafu 10,500 kati ya 124,500 hawajahakikiwa katika daftari la wastaafu la mfuko huo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 11, 2019 jijini Dar es Salaam, meneja kiongozi uhusiano na elimu kwa umma wa mfuko huo, Eunice Chiume amesema tangu Machi, 2019 mfuko huo ulisitisha ulipaji wa pensheni ili kushawishi wastaafu hao ama ndugu zao kujitokeza.

Eunice ametoa kauli hiyo alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communication’s Ltd (MCL) zilizopo Tabata Relini, lengo likiwa ni kuutambulisha mfuko, kuimarisha uhusiano.

“Kawaida ya uhakiki huo tunatoa mwezi mmoja ila safari hii tumetoa muda mrefu ili ikitokea sintofahamu waelekezwe kwa sasa mfuko ni mpya.”

“Lakini tunaamini wote tunaweza kuwapata kwa sababu asipotokea katika miezi tuliyotangaza, tunasimamisha malipo, akikosa ile pesa lazima ataibuka. Tukiona hajitokezi mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu, tunaanza kufuatilia sasa yuko wapi, ili tupate taarifa kama atakuwa amekufa au la,” amesema Eunice.,

Uhakiki huo ulianza Desemba, 2018 hadi Machi, 2019 baada ya kuunganishwa kwa mifuko uliotokana na mifuko ya LAPF, GEPF, PPF na PSPF.