Watanzania 5 milioni ndiyo wanamiliki vitambulisho vya Taifa

Wednesday June 12 2019

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma.Jumla ya Watanzania 5 milioni wameshapatiwa vitambulisho vya taifa huku 13 milioni vitambulisho vyao viko katika hatua za mwisho kutolewa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni leo bungeni Juni 11,2019 ambaye amesema hadi mwishoni mwa mwaka huu, vitambulisho 22.2 vitakuwa vimetolewa.

Alikuwa anajibu swali la Mbunge wa Buyungu (CCM) Christopher Chiza ambaye ameuliza serikali inampango gani kuharakisha zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa ili viwasaidie wananchi katika shughuli za maendeleo na kuondoa usumbufu kwa watu wa mikoani.

Naibu Waziri amesema utaratibu wa kuwapatia vitambulisho kwa haraka wananchi wanaoishi mikoa ya mipakani hautofautiani na maeneo mengine kinachotakiwa ni kufuata sheria na utaratibu lakini akasema wanampango wa kununua mashine nyingine kuongeza uzalishaji.


Advertisement