Watanzania wang'ara John Stephen Akhwari International Marathon

Muktasari:

  • Watanzania wameng’ara katika mashindano ya riadha yanashirikisha wanariadha zaidi ya 700 katika mbio za kolomita 21, kilomita 5 na moja huku wakiwaacha mbali wanaridha kutoka nchi jirani ya Kenya.

Arusha. Wanariadha wa Tanzania  wametamba katika michuano ya John Stephen Akhwari international Marathon baada ya kuwashinda Wakenya.

Mashindano hayo yaliyofanyika leo Jumapili Juni 9, 2019, Mwanariadha Emmanuel Giriki  alishinda kwa upande wa wanaume na Failuna Abdi kwa wasichana kushika nafasi za kwanza na kuwaacha mwanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya katika mbio za umbali wa kilomita 21.

Giriki ambaye anatoka jeshi la wananchi ametumia muda wa saa 1:01:50 huku Failuna kutoka klabu ya winning spirit akitumia muda wa Saa 1:12:20.

Kwa upande wa wasichana mshindi wa pili Judith Cherolo kutoka Kenya na nafasi ya tatu Magdalena Chrispin wa Tanzania.

Wavulana mshindi wa pili mshindi wa pili Stivin Huche na wa tatu Michael Joseph wote watanzania.

Kwa upande wa kilomita tano, Watanzania wameongoza kwa upande wa wavulana na mshindi ni  Marko Sylivesta,  nafasi ya pili  imechukuliwa na Mathayo Sombi na nafasi ya tatu ni Michael  Kishindi.

Kwa wasichana  mshindi ni Anastazia Dolomongo, wa pili Sara Hiiti na wa tatu Mary Naali.

Katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha wanariadha zaidi ya 700 katika mbio za kilomita 21, kilomita 5 na kilomita Moja, Mgeni rasmi ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.