Watu 37 wauawa nchini Chad

N'Djamena. Watu 37 wamepoteza maisha nchini Chad baada ya kuzuka kwa mapigano mapya ya kikabila, Mashariki mwa mkoa wa Ouaddie.

Rais Idriss Deby ametangaza kutokea kwa mauaji hayo, baada ya kuzuka kwa mapigano ya siku tatu katika mkoa huo unaopakana na nchi jirani ya Sudan.

Akizungumza na Wanahabari jijini Ndjamena, Rais Derby amesema mapigano ya kikabila nchini limekuwa sasa suala ambalo linatia wasiwasi, inaripoti RFI

Mapigano hayo yameshuhudiwa kati ya kabila la kuhamahama la Zaghawa linalofunga ngamia na wakulima kutoka kabila la Ouaddian.

Imekuwa ni wiki ya mapigano katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo na hospitali moja imeripoti kuwa watu walipoteza maisha ni 44.

Polisi waliokwenda kutuliza ghasia, walishambuliwa kwa risasi, suala ambalo Rais Deby amesema halikubaliki na amepanga kuzuru eneo hilo hivi karibuni.