Watu nane mbaroni kwa kufanya vurugu, kufunga barabara

Wednesday May 15 2019

By Hamida Shariff, Mwananchi [email protected]

Morogoro.  Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanane kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro- Dar es Salaam eneo la Maseyu mkoani hapa.

Vurugu zilizosababisha barabara hiyo kufungwa kwa muda zilitokana na mgogoro kati ya jamii ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Maseyu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Mei 16, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema kundi la watu hao lilifunga barabara saa 12:00 asubuhi wakishinikiza polisi kuwaachia huru wanakijiji wenzao wanne waliokamatwa Mei 13, 2019 wakituhumiwa kuchoma moto nyumba nne za mmoja wa wafugaji.

Amesema watu hao  walifunga barabara hiyo kwa kutumia mawe na magogo na kusababisha usumbufu kwa wasafiri na watu wengine.

Amesema watuhumiwa hao ambao hakutaka kuwataja majina kwa maelezo kuwa ataharibu uchunguzi, watafikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika.

 

 

Advertisement