VIDEO: Watuhumiwa wa mauaji ya watoto Njombe wafikishwa mahakamani

Tuesday February 12 2019

By Godfrey Kahango, Mwananchi [email protected]

Njombe. Watuhumiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wilayani Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakim Hakimu mkazi Njombe leo Jumanne Februari 12, 2019.

Leo ni mara ya kwanza wa watuhumiwa wa mauaji hayo yaliyotikisa mkoani Njombe kuanzia Novemba 2018 kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa hao ni Joel Nziku, Nasson  Kaduma, Alphonce Danda.

Nje ya mahakama hiyo ulinzi umeimarishwa kutokana na polisi kusambaa kila kona, huku msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi


Advertisement