Waziri Bashungwa kula sahani moja na viwanda vya nguo vilivyobinafsishwa

Tuesday June 25 2019

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma.  Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amesema mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa bajeti ataanza kushughulika na viwanda vya nguo ambavyo vilibinafsishwa lakini havifanyi kazi.

Kauli hiyo imetolewa na leo Jumanne Juni 25 2019 wakati akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

Amesema wamehamasika katika kilimo cha pamba ambapo kumekuwa na ongezeko kutoka tani 200,022 hadi 400,000 kwa msimu.

Amesema viwanda vya nguo vilikuwa 32 lakini hivi sasa viko vitano tu vinafanya kazi na kwamba wengi wamekiuka mikataba waliopewa juu ya ubinafsishaji.

Amesema Serikali itahakikisha kuwa vinafanya kazi ili kuongeza wigo wa soko badala ya kutegemea wanunuzi wa pamba pekee.

Kuhusu korosho, Bashungwa amesema kumekuwa na upotoshaji mkubwa ambao umesababisha dunia kuamini kuwa korosho ya nchini imeoza.

Advertisement

Amesema jambo hilo si kweli kwa sababu yeye baada ya kuapishwa alitembelea maghala yote ya korosho na kukuta iko katika hali nzuri.

“Sasa tunapoendelea kuwasiliana na wanunuzi duniani kuna watu wana bado wanaendelea kupotosha msinunue korosho ya Tanzania sio safi,” amesema.

Advertisement