Waziri Castico: Udhalilishaji watoto hautavumiliwa

Sunday June 16 2019

By Muhammed Khamis, Mwananchi [email protected]

Unguja. Waziri wa kazi uwezeshaji wazee wanawake na watoto, Maudline Cyrus  Castico amesema wakati umefika wa kuacha kuwavumilia wale wote wenye tabia ya kuwadhalilisha na kuwafanyia matendo maovu watoto.

Waziri huyo ameyasema hayo leo Jumapili Juni 16, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja  vya Kijiji cha SOS Mombasa mjini Unguja.

Amesema iwapo watoto watalindwa ni wazi kuwa jamii itaweza kutengeneza Taifa bora kwa maslahi ya wote.

Amesema bado kuna changamoto nyingi  wanazoendelea kukabiliana nazo watoto zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka.

Hata hivyo, amesema jamii haina budi kushirikiana na taasisi tofauti zinazojihusisha na usimamizi wa haki ya mtoto, kwa kuwa bila kufanya hivyo kunaweza kurudisha nyuma harakati za mapambano dhidi ya vita ya ukandamizwaji wa haki muhimu kwa watoto.

Amewataka pia watoto kutoyanyamazia matendo ya udhalilishaji na wawe wepesi kutoa taarifa pale yanapowakumba ili wahusika wachukuliwe hatua.

Advertisement

Advertisement