Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

Monday October 12 2015

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Abdalah Kigoda. 

By Emmanuel Mtengwa

Dar es salaam. Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki dunia leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge zinasema kuwa, Waziri Kigoda amefariki majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Appolo nchini India.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa kuhusu taratibu za msiba huo, ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na Serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadri zitakavyoendelea kupatikana.

Waziri huyo alipelekwa India kwa matibabu mapema mwezi Septemba

Advertisement