Waziri Mkuu Majaliwa atangaza kuahirishwa sherehe za Muungano, watu kupumzika kama kawaida

Muktasari:

Waziri Mkuu atangaza siku ya Muungano kuwa siku ya mapumziko kitaifa

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kesho Aprili 26 ni siku ya mapumziko na hakutakuwa na shamrashamra za sherehe za Muungano.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma, Majaliwa amesema kesho ni siku ya mapumziko kitaifa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Jumla ya Sh 988 milioni ambazo zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe hizo zimeokolewa na zitapangiwa shughuli nyingine,” amesema Majaliwa.