Waziri Mkuu Uingereza kushinikizwa ajiuzulu

Muktasari:

  •  Ofisi ya Waziri ya Mkuu haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na ripoti hiyo ya gazeti la Sunday Times

London, Uingereza. Mawaziri waandamizi wa Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May wanalenga kumshinikiza kiongozi huyo kujiuzulu.

May anakabiliwa shinikizo la kuachia madaraka kutokana na kusuasua kwa mkakati wake kuhusu Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit) baada ya makubaliano yake na Umoja wa Ulaya kukataliwa mara mbili na Bunge la nchi hiyo.

Gazeti la Sunday Times limewanukuu mawaziri 11 ambao hawakutajwa majina wakisema wamekubaliana kuwa May anapaswa kuondoka madarakani kwa sababu amegeuka kuwa kiongozi asiyetabirika na asiyeweza kuamua.

Taarifa hiyo imesema pia mawaziri hao wamepanga kesho kumtaka May aachie madaraka.