Yosso wa Arsenal waizamisha Bayern Munich Marekani

Thursday July 18 2019

Mshambuliaji chipukizi, Edward Nketiah jana alifunga bao la ushindi dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika na kuiongoza Arsenal kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya kujiandaa kwa msimu iliyofanyika California.

Arsenal ilimalizia pasi za haraka kuelekea golini katika dakika ya 88 kwa mchezaji mwingine chipukizi, Tyreece John-Jules kumburuzia mpira Nketiah, mwenye umri wa miaka 20, ambaye alifunbga kwa goti.

Arsenal imeshjinda mechi ya pili mfululizo katika ziara yake nchini Marekani, lakini mabingwa hao wa Ujerumani walikuwapa mtihani mgumu zaidi ya ule waliokutana nao kwa klabu ya Colorado Rapids inayoshiriki Ligi ya Marekani (MLS) waliposhinda kwa mabao 3-0 Jumatatu.

Klabu hiyo iliyomalizika katika nafasi ya tano ya Ligi Kuu ya England msimu uliopita walifunga bao la kwanza katika dakika ya 49 kwa bao la kujifunga katika mchezo huo uliofanyika mjini Carson na kuhudhuriwa na watu 26,700. 

Louis Poznanski alishindwa kumudu mpira pembeni ya goli na katika kujaribu kuuondoa akaishia kuuelekeza golini kwake.

Robert Lewandowski alisawazisha kwa mpira mzuri wa kichwa katika dakika ya 71 na kurejesha matumaini kwa mabingwa hao wa Ujerumani ambao msimu uliopita walitwaa mataji mawili.

Advertisement

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Serge Gnabry ndiye aliyepiga mpira wa juu ndani ya eneo la hatari la timu yake ya zamani na Lewandowski akaruka juu kuusukumia wavuni kwa kichwa.

Vijana wa Unai Emery walianza mechi hiyo ya pili nchini Marekani kwa nguvu licha ya kuwepo sakata kuhusu nahodha wake Laurent Koscielny ambaye amegomea safari hiyo kujaribu kulazimisha klabu yake imruhusu kuondoka.

Rome, Italia (AFP)

Beki Mholanzi wa kati, Matthijs de Ligt leo amesaini mkataba wa kuichezea Juventus kwa ada ya dola 84.2 milioni za Kimarekani, akitokea Ajax, mabingwa hao wa soka wa Italia wametangaza.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 amesaini mkataba wa miaka mitano.

Juventus ilisema katika taarifa yake kuwa fedha hizo zitalipwa katika kipindi cha miaka mitano ya fedha, pamoja na "gharama za ziada" ambazo ni euro 10.5 milioni.

Ada ya De Ligt inamfanya kuwa mchezaji ghali anayeshika nafasi ya tatu katika klabu ya Juventus akiwa nyuma ya Ronaldo (euro milioni 105 mwaka 2018) na Gonzalo Higuin (euro 90 milioni mwaka 2016).

De Ligt pia alikuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Manchester United, Barcelona na Paris Saint-Germain baada ya kuonyesha kiwango kikubwa ambacho kiliiwezesha Ajax kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Mchezaji mwenzake wa Ajax mwenye umri wa miaka 22, kiungo Frenkie de Jong, ameshajiunga na Barcelona.

De Ligt alicheza mechi 117 akiwa na na Ajax katika mashindano tofauti na kufunga mabao 13 na ndiye aliyefunga bao la ushindi mjini Turin wakati Ajax ilipoiondoa Juventus katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

De Ligt ameshaichezea timu ya taifa ya Uholanzi mara 17, akiunda beki pacha ngumu pamoja na Virgil van Dijk wa Liverpool.

Aliteuliwa kuwa nahodha wa Ajax Machi 2018 na hivyo kuwa nahodha mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika klabu hiyo.

De Ligt alisema Ronaldo alimshauri ajiunge na Juventus baada ya wawili hao kukutana katika fainali ya Ligi y Mataifa ya Ulaya mwezxi Juni na Ureno kuibuka bingwa.


Advertisement