Zitto amkabidhi Maalim Seif kadi namba 1, Babu Duni namba 10

Muktasari:

Vigogo mbalimbali  waliokuwa Chama cha Wananchi (CUF) leo

wamekabidhiwa kadi  za chama chao kipya cha ACT- Wazalendo


Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewakabidhi kadi za uanachama wa chama hicho waliokuwa vigogo wa Chama cha Wananchi (CUF) huku Maalim Seif Sharif Hamad akipewa kadi namba moja na Juma Haji Duni akikabidhiwa kadi namba 10.

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo,

Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.

“Nawashukuru sana kwa kukubali ombi letu kwamba tuje tuchangie nguvu katika chama cha ACT- Wazalendo na ninyi hamkuwa na ajizi mkatuambia njooni na haukuwa uamuzi wa viongozi pekee bali wa wanachama,” amesema Maalim Seif  

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea