Magufuli aahidi kuwalipa wakulima wa Korosho jimboni kwa Nape

Tuesday October 15 2019

 

By Haika Kimaro,mwananchi [email protected]

Lindi. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema wakulima 24 wa korosho kutoka Jimbo la Mtama ambao bado hawajalipwa fedha zao  msimu wa mwaka 2018/19 wataanzwa kulipwa wiki ijayo.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo Jumanne, Oktoba 15, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiwalala jimbo la Mtama wakati akienda wilaya ya Ruangwa kwa ziara yake.

“Hawa wakulima 24 ambao bado wanadai fedha zao tutawaletea kuanzia wiki ijayo, tutaanza kulishughulikia hili, tumetoa Sh30 bilioni zimelipwa lakini tutaongeza fedha nyingine ambazo nazo tutazilipa,” amesema Rais Magufuli

Kabla ya Rais Magufuli kutoa ahadi hiyo, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema mwawa jana korosho iliyumba na wakulima kwa kiasi kikubwa wamelipwa na wamebakia wakulima 24 ambao hawajalipwa.

“Wengine wote wamelipwa mpaka jana, hawa 24 ni wale ambao unakuta kuna matatizo ya akaunti ya hapa na pale, lakini mheshimwa Rias tunakushuru kwa kuingilia kati kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri,” amesema Nnauye

Katika msimu wa korosho mwaka 2018/19 kiasi cha tani 222,000  za korosho zilikusanywa zilizokuwa na thamani zaidi ya Sh723 bilioni.

Advertisement

Katika msimu mpya wa mwaka 2019/20 korosho kiasi cha zaidi ya tani  290,000 zinatarajiwa kukusanywa

Advertisement