Magufuli akataa ombi la waziri Mpina hadharani

Muktasari:

  • Aliomba jimbo la Kisesa lifanywe halmashauri kwasababu lina inadadi kubwa ya watu

Simiyu. Rais John Magufuli amelikataa ombi la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  ambaye pia ni mbunge wa Kisesa, kuhusu jimbo hilo kuwa halmashauri.

Rais Magufuli ameitoa kauli hiyo leo Septemba 9, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kisesa akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu.

Rais amesema Chato inawatu wengi  zaidi lakini haijatenga maeneo ya utawala.

Amesema sababu aliyoitoa Mpina ya uwapo wa watu wengi ni jambo lingine, “hata Chato ina watu wengi zaidi, lakini hatujawapa  halmashauri.”

Awali Mpina alimuomba Rais kuwa jimbo la kisesa ni kubwa na linaidadi kubwa ya watu hivyo anamuomba kuifanya halmashauri.