Majeruhi ajali ya moto Morogoro wabaki wanne hospitali

Wednesday September 11 2019

Meneja wa banki ya posta(TpB) Eliwangu Mwangama

Meneja wa banki ya posta(TpB) Eliwangu Mwangama akikabidhi Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo dawa na vifaa tiba kwa ajili wagonjwa ambao ni majeruhi wa ajal ya Moto Morogoro, mpaka sasa majeruhi wamebaki watatu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro. 

By Lilian Lucas, Mwananchi [email protected]

Morogoro. Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya amesema hadi leo Jumatano Septemba 11, 2019 saa 10 jioni katika hospitali hiyo wamebaki wagonjwa wanne tu wa ajali ya moto.

Ajali  hiyo iliyotokea Morogoro Agosti 10, 2019 katika mtaa wa Itingi, Msamvu barabara ya Morogoro-Dar es Salaam baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta. Watu 104 wamekufa kutokana na ajali hiyo.

Amesema katika hospitali hiyo  walilazwa majeruhi 18 na wameruhusiwa na kubaki wanne.

Amesema waliobaki wanaendelea na matibabu na kuwataka wadau mbalimbali kuendelea kutoa msaada baada ya Benki ya Posta (TPB) kutoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh3.9 milioni.

Advertisement