Bei ya kuku yapaa Dar es Salaam

Thursday August 9 2018

 

By Ephrahim Bahemu

Dar es Salaam. Wakazi wa Dar es Salaam hivi sasa wanakumbana na uhaba wa kuku jambo ambalo linasababisha bei ya kitoweo hicho kupanda kwa asilimia zaidi ya 300.

Bei ya bidhaa hiyo katika masoko mbalimbali jijini hapa ikiwa ni pamoja na soko la Kisutu, Tegeta, Ilala na Shekilango, kwa wauzaji wa rejareja bei inaanzia Sh7,000 mpaka Sh8,000 kulingana na uzito tofauti na bei ya miezi mitatu iliyopita ambayo wastani ulikuwa Sh6,000.

Wauzaji wa jumla bei imeongezeka nakuwa Sh7,500 kwa wastani kutoka wastani wa Sh5,500 kwa miezi mitatu iliyopita.

Muuzaji wa jumla katika soko la Kisutu Abdulla Mohammed alisema kuongezeka kwa bei kunachangiwa na uhaba uliopo na gharama kubwa za bidhaa hizo kutoka kwa wafugaji.

Neema Justine ambaye ni mfugaji wa kuku alisema sababu kubwa ya kupanda kwa bei ya kuku ni kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kama kuongezeka kwa bei ya madawa na chakula.

“Bei ya chakula cha kuku kwa gunia la kilo 50 imeongezeka kutoka Sh60,000 hadi Sh65,000 lakini bei ya dawa za chanjo imeongezeka ndiyo maana hata bei ya mayai imepanda sasa hivi,” alisema Justine.

Advertisement