Mechi ya watani wa jadi ni nderemo

16Mashabiki wa soka wakinunua jezi na vifaa vingine vya michezo kwenye mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika wiki iliopita. Picha na Michael Matemanga.

Muktasari:

  • Kila inapochezwa mechi ya watani wa jadi, uchumi na biashara jijini Dar es Salaam husisimka. Licha ya ushabiki na burudani inayopatikana wajasiriamali hutengeneza fedha  za kutosha.

Soka ni miongoni mwa michezo yenye wafuasi wengi zaidi duniani na nchini pia hivyo kutoa fursa nyingi za biashara zinazoingiza kipato cha uhakika.

Mapato yalitokana na kiingilio cha mlangoni kwenye mechi ili-yofanyika Februari 16 ni ushahidi wa hili.

Mashabiki 41,266 walio-ingia Uwanja wa Taifa kushudia mtanange kati ya Yanga iliyoi-karibisha Simba walilipa jumla wa Sh342.825 milioni.Mamlaka ya Mapato Tanza-nia (TRA) walipata chao, Yanga wenyewe, bodi ya ligi, Shirikisho la Soka (TFF), Baraza la Miche-zo Tanzania (BMT), Uwanja na Chama cha Mpira Dar es Salaam (DFRA) kila mmoja alipata mgao wake.

Ukiachana na taasisi hizo, kuna watu wananufaika pia kutokana na mchezo huo. Miongoni mwao ni wauzaji wa vinywaji hasa pombe, maji, soda hata ice cream.

Wapo wanaouza jezi, soksi, skafu au kofia.Wafanyabiashara hawa wapo nje ya uwanja wakiingiza fedha bila jasho kubwa. Ni kuwahudu-mia mashabiki wanaotaka kusu-uza nafsi zao kwa furaha walizo-nazo basi.

Pembeni ya Uwanja wa Taifa kuna baa tatu ingawa kub-wa na maarufu ni mbili ambazo hujaza watu wengi zaidi kila kunapokuwa na mchezo kati ya timu hizi kubwa zenye historia ya muda mrefu;

Simba na Yanga.Baa hizi ni Minazini na kwa Chichi ambazo zimegawana mashabiki. Minazini ni kwa mashabiki wa Simba wakati ile ya kwa Chichi ni mashabiki wa Yanga.

Timu inayoshinda hua-mua baa ipi iuze zaidi. Ndio hivyo, unywaji wa wateja hutege-mea ushindi uliopatikana.Ingawa mashabiki huwa hupa-ta vinywaji hata kabla mechi haijaanza nawao kuingia uwan-jani, lakini shangwe huwa kubwa zaidi wakishinda.

Kwa waliokuwepo wikendi ili-yopita walishuhudia furaha ili-yokuwapo katika baa ya Mian-zini ambayo mashabiki wa Simba ndio huitumia kudhidirisha jinsi wanavyosuuzika nafsi baad aya ushindi.

Msimamizi wa baa hiyo, Saddam Opiyo anasema huwa anatamani mechi ya watani hawa wa jadi iwepo hata kila mwezi.“Mauzo yanakuwa makubwa tofauti na siku zote.

Kwa siku za kawaida huwa tunauza kati ya kreti 15 mpaka 20 za bia lakini siku ya mechi ya Simba na Yanga tunauza zaidi ya kreti 600,” anas-ema Opiyo.

Kutokana na wingi wa wateja wanaokuwapo siku za mechi hizo, hata ajira za muda huon-gezeka kwani wafanyakazi 16 waliopo huwa hawatoshi hivyo kulazimika kutafuta wengine tisa.

“Kazi yao ni kuokota chupa na kuziweka sehemu salama. Kama unavyojua watu wakishakunywa wengine hutupa chupa ambazo ni lazima zikusanywe na kuwekwa sehemu yake. Mwisho wa siku kila mmoja huwa analipwa Sh15,000,” anasema Opiyo.

Siku zote za mechi, bila kujali aina ya wachzeaji waliopo kwenye kila timu, anasema huwa anaomba ushindi kwa Simba ili afanye biashara kwani baada ya mchuano mashabiki watarudi wengi zaidi hurudi na kununua vinywaji kwa wingi kutokana na furaha waliyonayo.

“Simba ikifungwa mashabiki wengi wakitoka uwanjani wanaondoka hapa wanakuja wachache na Yanga ikishinda basi inahamia kwa Chichi,” anasema Opiyo.

Mmoja wa mashabiki wa Simba aliyezungumza na Mwananchi katika Baa ya Minazini, Isaya Boniface anasema kunywa bia ni sehemu ya burudani na huwa wanakunywa zaidi Simba inaposhinda.

“Hii ndio starehe yetu. Kama unavyotuona, tunakunywa kabla ya kuingia uwanjani ili tukashangilia vizuri tena kwa mzuka mkubwa. hata tukipoteza inakuwa tofauti na yule ambaye hajanywa,” anasema Isaya.

Shabiki wa Yanga aliyezungumza na gazeti hili pia, Hassan Ally anasema hakuna kitu kizuri kama kunywa bia timu yako inapokuwa imeshinda.

“Yaani ukishinda halafu ukaja kunywa bia, huwa ni raha sana tofauti na ukifungwa, unakosa hamu nazo,” anasema Hassan.

Biashara uwanjani

Achana na foleni inayokuwepo siku ya mechi, kutokana mashabiki 60,000 wanaoweza kuujaza Uwanja wa Taifa, kuna biashara ndogondogo zinafanyika kutokana na umati unakuwapo.

Kutokana na jua kali jijini Dar es Salaam, maji ni biashara kubwa inayofanyika has akutoka kwa wafanyabiashara wadogo wanaokuwapo nje ya uwanja.

Kuna wauza ice cream pia ambao hunufaika zaidi kabla mechi haijaanza au wakati wa mapumziko kwani mashabiki wengi hupenda kutumia bidhaa hiyo wakiwa wanaangalia mpambano.

Vifaa vya michezo

Pamoja na ukongwe wa timu hizi hakun ailiyoweza kudhibiti uuzaji wa vifaa vyake iwe jezi, soksi, kofia au skafu ingawa wajanja w amjini wanaendele akunufaika na fursa iliyopo.

Wauzaji wa jezi hizo wanaingizia kipato kutokana na mauzo ya jezi za timu hizo hasa zinapokutana. Wafanyabiashara wa nje ya Uwanja wa Taifa huuza jezi moja kwa Sh15,000 ambayo ikinunuliwa kwenye maduka ya vifaa vya michezo hugharimu kati ya Sh25,000 mpaka 30,000.

Gharama kubwa ya jezi hizo katika maduka ya vifaa vya michezo yamesababisha wauzaji wa mitaani kunufaika. Mmoja wa wauzaji aliyekuwapo Uwanja wa Taifa wiki iliyopita, Mwajuma Athumani anasema kwenye mechi ya Simba na Yanga huuza kuanzia jezi 100 mpaka 300.

Mwajuma anasema kama timu mojawapo kati ya Simba na Yanga inafanya vizuri kabla ya mechi hiyo wanakuwa na uhakika mkubwa wa mauzo ya jezi kwani mashabiki wake huwa wanajiamini.

Muuzaji mwingine, Victor Patrick anasema katika mchezo wa Jumamosi ameuza jezi nyingi za mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere zikifuatiwa na za Emmanuel Okwi na kwa upande wa Yanga; Heritier Makambo na Ibrahim Ajib ndio waliomuingizia fedha nyingi.

“Huwa tunatamani mechi za Simba na Yanga ziwe kila siku kwa sababu tunauza sana jezi. Huwa kuna sehemu tunachukua kwa jumla (ingawa siwezi kusema kwa nani) halafu tunaziuza rejareja,” anasema Victor.

Aliyekuwa kaimu wa rais wa Simba ambaye kwa sasa ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Salim Abdallah lmaarufu kama Try Again amesema kuna mkakati wanaukamilisha ili mauzo ya jezi yainufashe klabu.

“Tunajua kuna uuzaji holela wa jezi ambao hauinufaishi klabu, kuna mpango mahususi sasa hivi tunaoushughulikia. Hivi karibuni tutautambulisha mpango wa uuzaji jezi zetu,” anasema Salim.