Mwalimu amvunja vidole mwanafunzi aliyefeli

Pamoja na adhabu ya viboko kupigwa marufuku katika nchi kadhaa duniani, huko nchini eSwatini), mwanafunzi wa miaka 12 katika shule ya msingi Mkhuzi amejeruhiwa baada ya kucharazwa kabora 25 na mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo alivunjujwa vidole na kupelekwa hospitali ambapo alifungwa majeraha aliyopata, huku mzazi wake akisema siku ya tukio binti yake alipata shambulizi la pumu na alitakiwa kwenda hospitali.

Mwalimu wake alitoa adhabu hiyo baada ya kutoa jaribio lenye maswali 25 na mwanafunzi huyo baada ya kukosa maswali yote alipewa adhabu ya viboko inayolingana na idadi ya maswali.

Pia wanafunzi wengine walipata adhabu ya viboko kwa viwango tofauti kulingana na idadi ya maswali waliyoshindwa ambapo wazazi wengi walipeleka malalamiko kwa uongozi wa shule baada ya watoto wao kuadhibiwa.

Mzazi wa mwanafunzi huyo alilalamika kuwa wajibu wa mwalimu huyo ni kumfundisha binti yake na sio kumvunja vidole akidai kitendo hicho kinamnyima sifa ya kuwa mwalimu huku akiwa na wasi wasi kama mtoto wake ataweza kuandika vizuri baada ya kujeruhiwa vidole.

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Manzini, Mlimi Mamba,alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusiana na suala hilo ambalo tayari limefikishwa mahakamani ambapo awali hospitali iligoma kutoa matibabu kwa mwanafunzi huyo na kusubiri kibali cha polisi.

Chanzo Times of Swaziland Swaziland(eSwatini),mwanafunzi wa miaka kumi na mbili katika shule ya msingi Mkhuzi amejeruhiwa baada ya kucharazwa kabora 25 na mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo alivunjujwa vidole na kupelekwa hospitali ambapo alifungwa majeraha aliyopata huku mzazi wake akisema siku ya tukio binti yake alipata shambulizi la pumu na alitakiwa kwenda hospitali.

Mwalimu wake alitoa adhabu hiyo baada ya kutoa jaribio lenye maswali ishirini na tano na mwanafunzi huyo baada ya kukosa maswali yote alipewa adhabu ya viboko inayolingana na idadi ya maswali.

Pia wanafunzi wengine walipata adhabu ya viboko kwa viwango tofauti kulingana na idadi ya maswali waliyoshindwa ambapo wazazi wengi walipeleka malalamiko kwa uongozi wa shule baada ya watoto wao kuadhibiwa.

Mzazi wa mwanafunzi huyo alilalamika kuwa wajibu wa mwalimu huyo ni kumfundisha binti yake na sio kumvunja vidole akidai kitendo hicho kinamnyima sifa ya kuwa mwalimu huku akiwa na wasi wasi kama mtoto wake ataweza kuandika vizuri baada ya kujeruhiwa vidole.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Manzini, Mlimi Mamba,alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusiana na suala hilo ambalo tayari limefikishwa mahakamani ambapo awali hospitali iligoma kutoa matibabu kwa mwanafunzi huyo na kusubiri kibali cha polisi.