NEMC yawaonya wanaotupa taka ovyo, halmashauri zisimamie

Thursday December 20 2018

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezitaka Serikali za Mitaa kuratibu na kusimamia utupaji taka kwenye maeneo yao na kuwaadhibibu wakataoabainika kukiuka sheria.

Licha ya utupaji, baraza hilo limehimiza urejelezaji wa aka ngumu zenye matumizi na manufaa mengi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi mkuu wa baraza hilo, Dk Samuel Gwamaka amesema utupaji ovyo wa taka ni kosa kisheria ambalo linapaswa kusimamia na wadau tofauti kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

“Ni marufuku kutupa ovyo taka ya aina yoyote au kumwaga kemikali, mafuta au mchanganyiko wenye mafuta kwenye chanzo au mkondo wa maji au sehemu yoyote,” amesema.

Alisema sheria inatoa adhabu kwa yeyote atakayekiuka ikimtaka kulipa gharama za kuziondosha taka husika na kulipa fidia kwa madhara yaliyotokea.

Licha ya Serikali za Mitaa, NEMC kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na udhibiti hufanya doria na ukaguzi wa mara kwa kuangalia jinsi hali ya uchafuzi wa mazingira maeneo tofauti.

Hivi karibuni, baraza hilo lilitembelea Mbezi Beach A kwenye Bonde la Mto Mbezi likiambatana na askari

polisi kuwadhibiti watupati taka wasiofuata utaratibu uliowekwa unaowataka kuzipeleka kwenye madampo.

Dk Gwamaka alisema kitengo cha mazingira na Serikali za Mitaa cha baraza hilo kitasimamia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa kuwahsirikisha viongozi wa maeneo yanayoathirika na utupaji taka huo.

“Mtu yeyote anayezalisha taka zenye madhara atawajibika kuzitupa na atabeba dhamana kwa madhara ya taka hizo kwa afya ya watu, viumbehai na mazingira pia,” alisema.

Halmashauri zote nchini, amesema zinajukumu la kuwatambua na kuzisimamia kampuni zinazokusanya, kusafirisha, kuteketeza na kuurejeresha taka.

“Si kila taka hutupwa, baadhi zinaweza

kuwa malighafi viwandani. Hata hivyo, sheria inazipa mamlaka Serikali za Mitaa kuzuia au kupunguza taka ngumu, taka vimiminika, gesi taka na taka zenye madhara,” alisema.

Mkuu wa kitengo cha mazingira wa Jeshi la Polisi, ACP Edward Balele wamejipanga vilivyo kuhakikisha utupaji taka unadhibitiwa kwa kufuata sheria kwa kila mtu kwa nafasi yake kuwajibika.

“Jeshi litafanya kazi kwa kuzingatia sheria kuhakikisha wanaokiuka utaratibu wanachukuliwa hatua stahiki,” alisema Balele.

Advertisement