Wadau utalii wanavyoitazama sekta wakati dunia ikivunja rekodi ya watalii 2018

Muktasari:

  • Kutokana na kutotangazwa vyema kwa vivutio vya utalii nchini, Waziri Kigwangalla amewatengua wajumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushindwa kuisimamia vyema menejimenti lakini wadau wa sekta hiyo wanasema kutekeleza ipasavyo jukumu hilo, ushiriki wa mamlaka nyingine pamoja na sekta binafsi unahitajika.

Wakati kukiwa na mwenendo usio-ridhisha nchini, takwimu za dunia zinaonyesha ongezeko la watalii mwaka jana zilikuwa kubwa kuliko ilivyo-tazamiwa.

Katika matarajio ya miaka mitatu mpaka 2018, Tanzania ilikusudia kuongeza idadi ya watalii inaopokea mpaka milioni tatu tatu kutoka milioni moja waliokuwapo mwaka 2015.

Kutokana na mwenendo huo usioridhi-sha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla alitengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yenye jukumu la kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

Wajumbe waliotenguliwa walipewa jukumu la kuisimamia TTB kuhakikisha inaongeza ufanisi wake ndani ya kipindi hicho.

Bodi hiyo ilimuhakikishia aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Profesa Jumanne Maghembe kuwa lengo hilo lingetekelezwa kwa mafanikio.Hata hivyo, takwimu zilizopo zinaonye-sha idadi ya wageni wanaotembelea vivu-tio vilivyopo haijafika milioni mbili mpaka mwaka jana.

Wakati tanzania ikishindwa kufanikisha lengo lake kutokana na sababu mbalimbali, dunia imefikisha lengo miaka miwili kabla ya muda uliotarajiwa.Katika mipango ya muda mrefu, Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) lilikisia idadi hiyo ya watalii ingekuwapo mwaka 2020. Idadi hiyo imeongezeka baada baada ya utalii wa Afrika kukua kwa asilimia saba ukiwa nyuma ya Mashariki ya Kati iliyokua kwa asilimia 10.

Ripoti ya shirika hilo zinaonyesha Ulaya ilipokea watalii milioni 713 ikifuatiwa na Asia milioni 343, Amerika milioni 217, Afri-ka milioni 67 na Mashariki ya Kati milioni 64 hivyo kuufanya mwaka 2018 kuwa wa pili kwa ubora zaidi tangu mwaka 2010. Mwaka 2019, shirika hilo linalenga kuon-geza uhamasishaji kwa kutoa elimu zaidi kwa wadau, kukuza ujuzi na kutengeneza ajira mpya nyingi.

Katibu mkuu wa UNWTO, Zurab Polo-likashvili anasema kukua kwa utalii kwa miaka ya hivi karibuni kunathibitisha kui-marika kwa sekta hiyo ambayo inawagusa wengi kadri siku ziendavyo.

Pololikashvili mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi, kuimarika kwa mataifa yanayotoa watalii wengi, usalama na utu-livu kwenye mataifa mengi yenye vivutio, kuboreshwa kwa huduma za usafiri na ura-hisi wa kupata viza, ni miongoni mwa mam-bo yatakayochangia kukua tena kwa utalii.

Wakati bodi ya wakurugenzi wa TTB inazinduliwa 2016, Tanzania ilikuwa inapokea wageni milioni 1.1 ambao mpaka mwaka 2017, takwimu za wizara zinaonyesha walifika milioni 1.3.

Kuongeza idadi hiyo mpaka milioni tatu ndani ya muda aliopendekeza Waziri Maghembe, mwenyekiti wa bodi, Jaji Thomas Mihayo anasema ilikuwa ni changamoto.

“Wakati tumeteuliwa tulikuta bodi haina fedha mpaka tulipopewa Sh2.2 bilioni ndipo tukaanza kuonekana. Kuongeza idadi ya watalii kwa zaidi ya asilimia 100 bila fedha za kutosha ungekuwa muujiza. Kiuhalisia, lengo tulilopewa lilikuwa halitekelezeki,” anasema Jaji Mihayo.

Baada ya kupata fedha hizo, anasema matumaini ni makubwa kwamba idadi itaongezeka siku za usoni kwani matangazo kadhaa yamefanywa kwenye masoko ya kipaumbele hasa China.

Vilevile, anasema kuna ushirikiano wa kutosha baina ya mamlaka zinazotangaza vivutio vilivyopo jambo litakalokuwa na manufaa makubwa huko mbeleni huku akiwataka Watanzania kubadili kubadili mzoea yaliyopo ya kutotembelea mikoani.

“Tunapaswa kuiga utamaduni wa Wachaga kwenda nyumbani kila mwisho wa mwaka ambao Wachina pia wanao. Hii husaidia kuchangamsha shughuli za kiuchumi,” anasema.

Alipokuwa anavunja bodi, Waziri Kigwangalla alisema imeshindwa kuisimamia menejimenti ambayo nayo inashindwa hata kuchapisha vijarida vya kuwekwa kwenye ndege.

“Kutangaza utalii unahitaji fedha, rasilimaliwatu makini na mikakati inayotekelezeka. Ukiwa hapa unaweza ukadhani watu wanaijua Tanzania kumbe hakuna,” anasema Jaji Mihayo.

Wadau wa utalii

Pamoja na nia nzuri ya Waziri Kigwangalla kutaka Tanzania ikaribishe watalii wengi kadri iwezekanvyo, baadhi ya wadau na wachambuzi wa sekta hiyo wanaona kuna changamoto kadhaa zinazopaswa kushughulikiwa na Serikali.

Mtafiti na mchumi mwandamizi, Profesa Samwel Wangwe anasema suala la kutangaza vivutio vya utalii si la TTB peke yao, lina wadau wengi wanaopaswa kushirikiana kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kutangaza utalii unahitaji fedha za kutafiti masoko yenye mvuto na kulipia matangazo husika. Utalii unahitaji miundombinu rafiki ya ufasiri kuanzia barabara kuu hata zinazoingia vilivko vivutio kama hifadhini na kwinginezo. Watu wenye ujuzi na weledi unaostahili wanatakiwa pia na hoteli zinazokidhi matarajio ya wageni, haya yote si majukumu ya TTB,” anasema Profesa Wangwe.

Kutoka tulipo, anasema ipo haja ya kuwa __ sera mpya ya utalii itakayotoa muongozo kwa kila mdau kutekeleza majukumu yake. “Ukiwaambia TTB walete watalii milioni tatu itawatoa wapi?” anahoji.

Aliyekuwa ofisa mtendaji mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Latifa Sykes anasema licha ya fedha kwa ajili ya utafiti, teknolojia ni muhimu pia kufanikisha kutangaza vivutio vilivyopo.

“Itapendeza kama bodi ya wakurugenzi wa TTB itakuwa na walau asilimia 50 ya wajumbe wake kutoka sekta binafsi ambao wanaijua zaidi sekta hii. Watasaidia kushauri mambo mengi. Siku hizi utalii hautangazwi kwa maonyeho, teknolojia inatumiza kuwafikia watu wengi duniani,” anasema Latifa ambaye pia aliwahi kuwa mtendaji wa chama cha wawindaji.

Miongoni mwa kero zilizopo, Latifa anasema ni namna watalii wanavyohudumiwa hasa wanapoondoka uwanja wa ndege ambako wakiwa na kinyago walichokinunua nchini wanatakiwa kukilipia. Kuna tozo nyingi nyingine zinazoifanya Tanzania kuwa kituo ghali cha utalii ikilinganishwa na nchi jirani.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Deogratius Mahangira anasema licha ya kufufliwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kurahisisha usafiri, kuna haja ya kurekebisha kodi na tozo zilizopo kwenye sekta ya utalii.

“Miundombinu iboreshwe ili wadau wengine washirikiane vyema na TTB kuhamasisha utalii. Hoteli zano zitoe huduma zinazokidhi matarajio ya wateja,” anasema Dk Mahangira.