DONDOO: Kushiriki tendo huchelewesha ukomo wa hedhi

Wanawake wanaoshiriki tendo la wana nafasi kubwa zaidi ya kuchelewa kukoma hedhi wakilinganishwa na wenzao, wenye umri sawa, ambao hawafanyi hivyo, utafiti unaonyesha.

Ufanyaji wa tendo hilo walau mara moja kwa wiki, watafiti wanasema huchelewesha ukomo wa hedhi kwa asilimia 28 ikilinganishwa na wanaoshiriki chini ya mara moja kwa mwezi, unasema utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Royal Society Open Science.

Tofauti iliyopo, utafiti huo unasema ni mwili kuitikia vichocheo vya mfumo wa uzazi.

“Kama mwanamke hashiriki tendo la ndoa mara kwa mara anapokaribia umri wa kati, mwili hautapokea taarifa za uwezekano wa kushika ujauzito,” anasema

Megan Arnot na Ruth Mace kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi London waliofanya utafiti huo.

Hii ndio kusema, wanawake walioolewa huchelewa kukoma hedhi wakilinganishwa na weye umri sawa ambao wanaishi peke yao kutokana na ushiriki wao wa kufanya mapenzi. (AFP)