Kampuni ya Uingereza yagundua dawa ya tezidume

Friday October 18 2019

 

Kampuni ya Astra Zeneca ya nchini Uingereza, imegundua dawa inasemekana kuwa na uwezo wa kutibu saratani ya tezidume hivyo kutoa matumaini kwa walioathirika nao. Dawa hiyo ijulikanayo kama Olaparib ipo kwenye hatua ya majaribio na itaingia sokoni miaka michache ijayo.

Kukabiliana na maradhi hayo, watafiti wanasema dawa hiyo huua seli za saratani na kuzirudishia virutubisho vinavyohitajika seli zilizobaki.

Kwenye majaribio ya awali yaliyoanza mapema Julai, watafiti waliitumia dawa hiyo ambayo hujulikana pia kama Lynparza na kuishindanisha na zinazotumika zaidi hivi sasa; abiraterone na enzalutamide na ikaonyesha matokea mazuri.

Advertisement