Kula tango kila wakati likusaidie kutoa sumu mwilini

Friday August 10 2018

 

By Hadija Jumanne

Tango ni miongoni mwa matunda yenye maji mengi na linabeba virutubisho vingi vikiwamo vitamin K,B,C, potassium na manganizi ambayo kwa pamoja huondoa sumu mwilini.

Hata hivyo, matunda ni kinga kwa afya ya binadamu na mtu anayekula matango mara kwa mara kwa kutengeneza juisi au kuchanganya kwenye kachumbali bila kumenya maganda yake, anakuwa amebeba virutubisho vizuri.

Pamoja na kukosa utamu, lakini ni vizuri ikafahamika tunda hili linasifa kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku kwa sababu tango moja lina vitamin B, C, K, B1, B2, B3, B4, na B6 madini ya chuma, potasium na zinki. Wataalamu wa masuala ya lishe wanasema tango husaidia tatizo la midomo kukauka kwa kupaka kipande cha tango kwenye lipsi za mdomo.

Tango pia huzuia kusukari, huboresha mfumo wa damu na kuondoa kolesto mwilini huku tunda hilo likisaidia kutunza ngozi na ukuaji wa nywele.

Faida nyingine ya kula tango ni chanzo kikubwa cha vitamin B, husaidia mwili kuongeza maji, huimarisha mmeng’enyo wa chakula mwilini na kuzuia saratani.

Mtu anayekula tango mara kwa mara linamsaidia kuboresha viungo vya mwili na kumuondolea maumivu na huondoa pia harufu mbaya ya kinywa.

Tango lina anti-inflammatory flavonol inayosaidia kutoa kinga ya ubongo na kumfanya mtu awe na kumbukumbu nzuri. Mbali na hilo, tango pia linasaidia kupunguzia hatari ya kupata saratani ya matiti na sehemu za uzazi na hupunguza msongo wa mawazo kwa sababu lina vitamin B, B1,B5 na B7 ambazo hupunguza tatizo hilo.

Kwa upande wa vipodozi, tango hufanya ngozi iwe laini na kukuza nywele kwa haraka na hutumika pia kutoa alama nyeusi chini ya macho lakini husaidia kupunguza uzito wa mwili.

Advertisement