Mc Pilipili kufunga ndoa Juni 25

Saturday May 25 2019

 

Mchekeshaji, Emmanuel Mathias maarufu kwa jina la ‘MC Pilipili’, amesema kwamba anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake, Cute Meena Juni 25, mwaka huu.

Kuhusu tarehe ya harusi, alisema wakazi wa Dar es Salaam watashuhudia harusi hiyo Juni 25 mwaka huu, huku ratiba katika mikoa mingine ambapo harusi hiyo imepangwa kufanyika ikiwemo Arusha, Dodoma, Geita na Mwanza kutangazwa hapo baadaye.

Ameliambia Mwananchi kuwa, maandalizi ya harusi yake yanaendelea na kwa Dar es Salaam itafanyika katika Uwanja wa Taifa.

“Maandalizi ya harusi yanaendelea vizuri. Unajua harusi ya MC wa taifa lazima ifanyike Uwanja wa Taifa,” alisema.

Hata hivyo, amesema hajapanga tarehe rasmi kwa sherehe za mikoani kwa kuwa bado anaendelea na vikao vya harusi.

“Kuna baadhi ya mambo yanaendelea yakikamilika nitatoa ratiba ya sherehe nzima katika mikoa tarajiwa. Maandalizi yanakwenda vizuri ninaamini itakuwa sherehe ya kipekee kuwahi kutokea nchini.”

Advertisement

Advertisement