Ndani ya boksi: FA, kweli dunia bila totozi ni uboya

Saturday December 14 2019

 

By Dk Levy

Mwanzoni mwa utawala wa JK, kuna wakati kila kijana alitamani Uzitto Kabwe. Kwa sababu siasa za nchi hii zilisimama kwenye koo lake. Alikuwa mwamba angali mdogo sana akavuka mipaka ya siasa na kuwa kivutio kwa vijana, watoto na wazee. Katika tatu bora ya wanasiasa maarufu alikuwemo. Pamoja na uchanga wake wakitajwa wanasiasa kwa wakati ule angeanza Jakaya, Lowassa kisha Zitto.

Baadaye kila mtoto alitamani Usteven Kanumba ni baada ya kulishikilia mateka soko lote la filamu. Jamaa akiwa bado kinda kabisa kiumri tayari jina lake lilisambaa kama ukoka Bongo na Afrika. Akawa mkubwa na kujijengea himaya ya kuumba waigizaji. Miss au mrembo yeyote aligeuzwa staa wa filamu kupitia mikono salama ya Kanumba.

Baadaye ukaja ugonjwa wa ‘Udiamond Platinumz’. Dogo anayeendesha bajaji au bodaboda alitamani kuwa Diamond. Mikimbizo ya hatari katika kuwanyoosha watoto wazuri mjini. Bandika bandua ya ngoma za msela wa Tandale. Kuingiza mkwanja chekwa na kusukuma ndinga kali ukawa sehemu ya uchizi kwa madogo mitaani.

Vijana watatu hawa wa kiume wakawa mfano wa mafanikio kwa wanasiasa, waigizaji na wanamuziki. Sijamuongelea 255 Champion Boy Mbwana Samatta. Lakini kwa upande wa totozi kunahitaji msukumo kidogo. Hakuna mizuka ya totoz kutamani kuwa Flaviana Matata, huoni wakitamani Ujokate wala kushitushwa na dili za Vanessa Mdee.

Wakati Nandy ‘anapushi’ ndinga anayotaka akila na kulala atakapo, akikimbiza jukwaani na mitandaoni kwa ngoma kali zinazoongozana kama msafara wa rais, jamii ya kike ya sasa haina mizuka na mafanikio hayo kuliko penzi lake kwa Billnass. Wanatamani kusikia matukio yake na Billnass zaidi. Umbea kwao ni bora zaidi.

Wema alipokuwa mwenyeji wa korido za Kisutu kisa picha na video za utupu. Baada yake kukawa na lundo la matukio hayo kutoka kwa warembo wengi mjini. Kwenye matukio ya ajabu ndiko walio wengi huiga haraka Wenye kazi bora hawana mvuto kwa wenzao.

Advertisement

Matukio yanayompa jina zaidi Aunty Ezekiel ni tofauti na ubora wa kazi za Riyama Ally asiyetajwa sana. Huhitaji majaji wakuambie Riyamah Ally ni zaidi ya Aunty kwenye uigizaji. Ushamtazama Thea akiigiza? Akikasirika kama kazi. Akicheka kama jukumu. Na kushangaa kiwito? Anavaa uhusika utadhani kwenye filamu ndiye halisi wa mtaani huku ni feki. Lakini yeye na Jack Wolper walinganishe kwa ukubwa wa majina yao. Unaweza kudhani Thea ni shabiki wa Jackline Wolper.

Matukio ya ‘kutrendi’ yanapaisha majina ya wasanii kuliko ubora wa sanaa yao. Wakati zamani tuliishi vile dunia inataka. Sasa dunia inaenda vile watu wanavyoishi. Usawa kimekuwa kitu adimu sana. Tunatengeneza majina ya wasanii kwa matukio badala ya kazi zao.

Ajabu ni kwamba jamii ya kike ndiyo inayowapa tuzo wasanii wetu, nguvu na kuwaunga mkono zaidi. Msichana ni kiumbe pekee anayeweza kuonyesha hisia, akadondosha chozi kwa furaha ya kumuona ‘laivu’ msanii anayempenda, kununua kazi zake na kumpigia kura.

Muziki na sanaa ya uigizaji ziko chini ya kwato za kina mama ndiyo wanaoimbiwa na wanaoguswa na kitu kinachoigizwa na msanii zaidi ya mwanaume. Ukitaka sanaa yako ifanikiwe haraka teka jamii ya kike. Ukifanikiwa, kazi zako utawauzia hata masela.

Lakini pamoja na yote. Mchawi wa mwanamke ni mwanamke. Wanaowapa umaarufu mastaa wa kiume ni jamii ya kike na sasa wao ndiyo wamechagua kupenda matukio ya ‘kiki’. Wao ndiyo wako bize mitandaoni kuwaongelea zaidi kina Hemed PhD kuliko Monalisa. Endapo madem wataamua kubebana, masela watatafuta njia wasiione.

Mwana FA hakuwa bwege alipowaimbia ‘Yaani shwari hamna shari’. Mimi na mabinti damu damu... Kweliii... Sababu zipo wazi mwenye macho aone eeh... Huhitaji kutumia darubini wala ramli kujua kila mtaa, baa na biashara, zinapambwa na warembo. Hawa ndiyo wanaomiliki uchumi wa dunia kwa mlango wa uani.

Wengine ndani jinzi, wengine ndani ya sketi na wengine mini au magauni ya vitambaa vyepesi. Mradi istizahi wanipore uhuru wa nafsi. Wale wabunifu wa mavazi ya viumbe hawa wametumwa. Wakati mwingine tusilaumu wenye kuvunja ndoa kibwege. Wanahitaji msaada wa maombi yetu.

Kuna werevu wa ajabu kwenye mambo mengi baa. Kuna totozi maisha yao yote ni baa. Anaamka na hengova na breki ya kwanza baa kunywa supu kisha anazimua. Kukiwa na madanga yanayoeleweka ndo harudi nyumbani. Libeneke linaendelea hapo hapo mpaka usiku mwingine unaingia. Wanamaliza ‘tishu’ tu kwenda msalani kila saa.

Wa kwenye mabaa ukimuita mmoja wanakuja 11. Hawana haya wala soni. Wengi hawana kazi na mavazi yao makubwa ni vijora na madera. Mawigi yamechakaa kiasi cha kutoelewa kama ni kichwa cha kike au dafu la Maneromango.

Wengi wao huzalia nyumbani. ‘Hawanaga’ boy friend wala mchumba. Kanyaga twende.

Hawanipi shida sio balaa.

Na zaidi nawapenda mabinti watundu na mikogo ya kifisadi usio makini inapotosha...Unaona shanga za miguu unaita vikuku.

Ingawa kwa wenye ufahamu ni potofu. Ukipishana nao njiani, kama una uchungu na pesa au ndoa yako usigeuke nyuma kuwatazama. Utembeaji wao ni ndugu moja na matumizi mabaya ya pesa kwa wanaume.

Watoto wa Kibongo hakuna mchezo. Kuna Walatino, Waafrika na wa Santa Domingo...Kuna mpasuo toka chini hadi kando ya kiuno.

Milango wazi kwa yeyote aliye na mdomo.Wanajiremba ili watazamwe. Watamaniwe, wapendwe, watongozwe na mwisho wahongwe. Kwanini uhangaike tafuta hela maana mdomo tu hautoshi kwa viumbe wa leo.

Sijapoteza macho kuangazia warembo. Nashukuru Mungu. Nakosa uzalendo nionyeshwapo miguu. Napata uchizi wa mtima. Choma fedha na muda sioni balaa. Ndo maana nikizipata naruka sana. Siku nikikosa ‘simaindi’ kwa sana. Nikipata tena naruka tena. Natumai sijifunzi hasara. Ni hadithi na si biashara. Ukishindwa Inshallah

Kuna totozi huwezi kuwaona kwenye Bongofleva, Bongo Movie wala siasa. Huwakuti kwenye shoo zenu na mabaa yaliyotapakaa kila kona. Wako vizuri umbo, sura na kiuchumi. Kuna mitego ya khanga.

Hawa wa kanga moko uko nao sana Uswahilini huku. Asubuhi anaamka na kutembea bila soni mpaka nyumba ya tatu ana kanga moja. Kila kitu unaona bila kuhitaji usaidizi. Ni mke wa mtu na kitu cha kawaida, kama mgeni utashangaa mtaa mzima.

Ona visa kwenye mitindo ya vichwa. Huyu kanyoa na kuweka rangi, yule kasuka na mwingine wigi. Anuani pepe za mitandano na simu zinawehusha. Wanachati hata kwenye bodaboda iliyo kasi. Wamejibinua kama kimitego.

Kuna wadada, wamama, masista du wote wapenzi. Mama anadanga, mtoto anadanga, wifi anadanga, mke mdogo anadanga, mkwe anadanga vilevile. Wana nataka sitaki. Kama wewe sio kamanda unaachia ngazi.

Kuna wale wa magroup ya whatsApp na ‘upumbavuni’ insta. Omba majina. Amina kawa Amayna, Naima, Clara na Rayah. Kuna Tayana, Aneth hata Bongo kuna Aaliyah? Candy, Nicole, Unice au labda Marayah. Sikitu hataki jina na Asia anaitwa Eshia. Sasa omba namba uombwe pesa mkutane. Kwenye ‘magrupu’ ndo rahisi kama unanawa vile. Bila madem dunia ingekuwa ya kidwanzi sana. Hata utafutaji usingekuwepo. Unatafuta mali ukale na mbweha? Pamba hazibani ni hatari... Ni makusudi tuone mstari wa kufuli... Lengo lao tupagawe na kuzisusa familia zetu. Msiache washikaji wawafanye watumwa nyie ndio mama na anayewaponda apate laana.

Advertisement