Ommy Dimpoz ‘atesti’ koo lake Oman

Saturday March 9 2019

 

Baada ya kuugua kwa takribani miezi minane, mkali wa Nai Nai, Ommy Dimpoz ametumbuiza nchini Oman mwezi uliopita.

Katika mtandao wa Instagram, mwanamuziki huyo ameposti kipande cha video akiwa jukwaani katika moja ya maonyesho ya Alikiba.

Amesema Alikiba ambaye anafanya naye kazi katika lebo moja ya Rockstar 4000, alimpa nafasi ya kupanda jukwaani kwa mara ya kwanza tangu arudi mtaani.

Huku akimtania Steve Nyerere alisema amepata nafasi ya kujaribu vocal zake, moja kati ya utani uliotengenezwa mitandaoni.

Steve Nyerere naye alimjibu kwa utani kuwa kwa sababu amepona atamwalika akaimbe katika sherehe yake ya kuzaliwa.

Advertisement