Q.Chilla: Sina jipya kwa sasa

Saturday December 8 2018Q.Chilla

Q.Chilla 

Msanii Abubakar shaaban’Q.Chief’, amesema kwa sasa hana jipya na ndio maana hasikiki kwenye vyombo vya habari.

Mkali huyo wa vibao kama ‘Ulinizaa Wewe’, Sungura, Tutaonana Wabaya alisema hayo katika mahojiano yake na Mwananchi lililotaka kujua sababu za ukimya wake ikiwa ni miezi mitano tangu aachie kibao cha Chuma Kisamvu.

Katika maelezo yake Q Chilla alisema siyo kila wakati mtu anatakiwa azungumze isipokuwa pale tu anapokuwa na jipya la kufanya hivyo.

“Sasa mimi kwa sasa sina jipya lolote nililofanya kwa nini nizungumze ovyo, nimeamua kukaa kimya kwanza japokuwa nataka mashabiki wangu wajue ukimya wangu una kishindo,” alisema msanii huyu ambaye Mei mwaka huu alitangaza kutaka kuacha muziki baadaye walijitokeza watu waliojiita wadau na kufanikiwa kumrudisha katika muziki.

Q Chief alivuma kimuziki katikati ya miaka ya 2000.

Advertisement