Sababu shule za Dar kujinasua mkiani

Tuesday February 12 2019

 

By Bakari Kiango, Mwananchi [email protected]

Mwaka 2016 Mkoa wMwaka 2016 Mkoa wa Dar es Salaam ulitoa shule sita katika orodha ya shule 10 zilizoshika mkia katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.a Dar es Salaam ulitoa shule sita katika orodha ya shule 10 zilizoshika mkia katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne.

Shule hizo zilikuwa; Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Kidete na Somangila.

Mwaka 2017 shule nne zikajinasua, mbili zikabaki ikiwamo moja mpya na nyingine iliyoendelea kuburuza mkia tangu 2016. Iliyoendelea kubaki ni Shule ya Sekondari Nyeburu huku ingizo jipya likiwa Shule ya Sekondari Furaha.

Kasi ya Mkoa huo kuondokana na aibu ya matokeo kwa shule zake, imejidhihirisha tena katika matokeo ya mwaka 2018 yaliyotangazwa hivi karibuni.

Hakuna shule ya Serikali iliyoingia katika orodha ya shule kumi za mwisho.

Kilichoinasua Dar

Ofisa elimu mkoani humo Hamis Lissu, anasema jambo la kwanzwaliimarisha uongozi na usimamizi kwenye shule hizo, kwa sababu waliokabidhiwa jukumu za kuzisimamia ambao ni walimu wakuu walishindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo suala la mahudhurio kwa wanafunzi na ufundishaji. “Tuliamua kuwabadilisha walimu hawa. Jambo la pili tulilolifanya ni kuongea na walimu ,pamoja na wanafunzi kuhusu wajibu wa kutambua majukumu yao,”anasema

Lissu anasema walimu hao waliwaeleza changamoto wanazokabiliana nazo, katika utekelezaji wa majukumu yao. Zile changamoto zilizokuwa ndani ya uwezo idara ya elimu zilitatuliwa kwa haraka.

“Moja ya changamoto waliotueleza ni madeni, walimu wetu hawa walikata tamaa kwa sababu wanadai madeni ya muda mrefu ya likizo, matibabu na nyongeza za mishahara. Yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wetu yalitatuliwa na ngazi ya wakurugenzi.

“Kwa upande wa wanafunzi nidhamu wao ilishavurugika kutokana na usimamizi wa mbovu wa shule husika.Tuliwaagiza walimu wakuu wateue walimu wa nidhamu ili kusimamia suala hili, anasema na kuongeza:

Wanafunzi wanaosoma shule wanakaa mbali na makazi yao, lakini tulikaa na kuzungumza nao na walirudisha nidhamu ikiwamo kuwahi shuleni ndio sababu mojawapo ya kujinasua kutoka katika shule zilizoshika mkia”anasema Lissu.

Advertisement