Shughuli ya Man United Dubai si mchezo

Monday January 14 2019

 

Manchester United jana walikuwa na kibarua cha kuonyeshana kazi na Tottenham Hotspurs ikiwa ni mchezo wa kwanza mkali kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye amekamata mikoba ya Jose Mourinho aliye benchi kwa sasa.

Solskjaer amesimamia timu hiyo vizuri. Tangu aichukue yenyewe ni kupiga mabao tu, imeshinda mechi tano za Ligi Kuu na Kombe la Emirates. Achana na matokeo ya jana usiku.

Lakini kabla ya mchezo wake huo wa jana, aliipeleka Manchester United kwenye kambi ya mazoezi kule Dubai. Walijichimbia kama siku nne hivi kujinoa kikamilifu.

Unaweza kusema kuwa walikwenda kula bata. Lakini la hasha, halikuwa bata unaambiwa. Ilikuwa ni tizi la kufa mtu kwa kwenda mbele pamoja na Solskjaer kuzungumza na wachezaji mmoja mmoja.

Baada ya timu hiyo kucheza na Reading Kombe la Emirates kwenye Uwanja wa Old Trafford, walikwea pipa kwenda Dubai kujichimbia kwa mazoezi makali kabla ya kuivgaa Tottenham.

Kwanini Solskjaer aliwapeleka Dubai?

“Nilitaka kutumia nafasi ya kuwafahamu wachezaji mmoja mmoja kwa kuwa kwa muda sasa tumekuwa tukifanya kazi lakini tulikuw ahatufahamiani,” anasema

Solskjaer. “Hata hivyo, kingine hatukuwahi kuwa na mazoezi ya nguvu kama haya tuliyofanya. ”Ilikuwa muda mzuri kwa kila mchezaji kujitengeneza, kujiweka fiti, Kama kuna mchezaji alikuwa akidhani ilikuwa mapumziko, ilikuwa kosa, tuylikuwa pale kutengeneza muunganiko, tulifanyia kazi fiziki na zaidi kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu,”

Solskjaer anasema kuwa ni vizuri kwa timu kufanya mazoezi makali ya kujijenga na kujiweka fiti inapotokea kuna nafasi ya muda mrefu kusimama na kwamba anataka kuhakikisha kila mchezaji anacheza kwa nafasi yake.

“Nimefurahi kuwa nao pamoja,” anaongeza. “Wanataka kujifunza, wanataka kubadilika na hilo ndilo linalotakiwa kwa kila mchezaji. Kama mchezaji anahasira, kama mchezaji ni mpole, kila kimoja kinafanyiwa kazi.”

Kilichojiri

Solskjaer alilazimika kumrudisha nyumbani Marcos Rojo kutokana na kuwa majeruhi. Kwa kuwa katika kambi ile ilikuwa kazi kazi, mchezaji huyo alishindwa kuhimili na kulazimika kurudishwa nyumbani akajiuguze. Mchezaji huyo amekuwa katika wakati mgumu kutokana na majeraha hayo kwani katika Ligi Kuu msimu huu amecheza dakika 103 pekee.

Solskjaer anasema kuwa alimchukua Rojo kwenda naye Dubai, lakini kwa jinsi mazoezi yalivyokuwa magumu alishindwa kutokana na kuwa majeruhi.

Rojo aliliambia gazeti la Manchester: ‘Kinachoniuma ni kwamba huu ni msimu wa pili nimekamatwa na majera. ‘Nimeshindwa kucheza kwa muda mrefu, kitu kinachoniuma kwamba ninalazimika kutengwa na klabu ili nijiuguze kwanza. Hali iko hivyo na sina jinsi, hiyo ndio soka.

Baada ya kambi aliwaambia wachezaji

“Nimefurahi, tumefanya mazoezi ya pamoja lakini ninachotaka kuwaambia ni kwamba mpango wangu ni kila mchezaji apate nafasi ya kucheza. Ukionyesha uwezo kwanini nikuweke nje.

“Katika falsafa yangu, hakuna mchezaji staa, ninachoamini ni kuwa kila mchezaji ana nafasi yake. Ninawataka muwe huru, sitaki makundi na kila mmoja atacheza ni suala la muda.

“Ninachosisitiza ni amani katika vyumba vya kubadilishia pale Old Trafford.

“Nimekutana nanyi kwa uwingi wenu na nimezungumza na mmoja mmoja n katika chakula hiki cha usiku, tule tukijua tunaondoka Dubai tukiwa na kazi kubwa mbele yetu.” Kati ya mambo ambayo kocha huyo amefanikiwa ni kwa wachezaji kujitambua na kujituma kwa kila mchezaji.

“Nawashukuru kwa jitihada zetu, mmeonyeha bidii ya hali ya juu hadi hapa mlipofikia,” anasema.

Advertisement