Super D, natamani ngumi ziwe matawi ya juu

Monday October 1 2018Rajabu Mhamila ‘Super D’

Rajabu Mhamila ‘Super D’ 

By Imani Makongoro, Mwananchi

Wadau wengi wa michezo hapa nchini wamekuwa wakijihusisha karibu na michezo lakini wanashindwa kusonga mbele kutokana na msukumo wa jamii katika michezo kuwa mdogo inayopelekea kukosa wadau kudhamini michezo.

Kocha wa kujitegemea wa ngumi anayefundisha klabu ya Ashanti ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Rajabu Mhamila ‘Super D’ amekuwa ana programu maalumu ya kuwafundisha vijana ambayo huwa anaiendesha katika ufukwe wa bahari ya Hindi, sehemu ya Coco Beach.

Super D anasema alianzisha program hiyo ili kutumia vizuri kipaji chake alichopewa na Mungu ili wengine wafaidike.

“Nimeona vijana wengi hawana kazi wapo tu mitaani na wana vipaji sasa nafundisha kwa kujitolea ili kuibua vipaji vyao na hatimaye waweze kutimiza malengo yao katika maisha,” anasema Super D kocha wa ambaye aliwahi kuchezea klabu ya zamani ya ngumi ya Simba Boxing Jijini Dar es Salaa.

Super D ambaye kitaaluma ni mwandishi wa Habari na mpiga picha anasema anaamini vijana wengi wanaweze kufika mbali kupitia mchezo huu kama wakiwezeshwa.

Anasema alianza programu yake ya ufukweni na vijana wachache lakini idadi yao huwa inaongezeka.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.

Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka.

“Inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuria.

Anasema mabondia aliokuwa nao hadi sasa wanawafuatilia kwa makini kuona wanafikia wapi na si kuwaacha njiani.

Advertisement