Ungo umembeba Callisah ushindi Mr Africa - Makeke

Saturday December 8 2018

 

Mbunifu wa mavazi, Jocktan Makeke amesema amefurahi vazi la ungo kuchangia kumpa ushindi mwanamitindo maarufu Callisah ambaye ameshinda katika mashindano ya Mr Africa International.

Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Nigeria na Calissah aliibuka mshindi huku picha aliyovaa vazi la ungo maarufu kwa jina la ‘Lupahero’ ambao ni ubunifu wa Makeke likiwa vazi rasmi la mwanamitindo huyo.

Akizungumzia hatua hiyo, Makeke amesema anajisikia faraja kwa vazi hilo kuendelea kuchanja mbugo na kueleza kuwa pia limeingia katika kumi bora ya mavazi katika tasnia ya ubunifu mavazi.

“Awali wakati Callisah amekuja kwangu na kuchagua hilo la ungo, niliona ushindi ukiwa unanukia kwake kwa kuwa ni vazi ambalo lina mvuto machoni mwa watu,” amesema Makeke.

Advertisement