Breaking News

Watumiaji wa Whatsapp wafikia bilioni mbili

Saturday February 15 2020

 

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu ya Whatsapp, tambua kuwa mnaotumia mmefikia bilioni mbili kote duniani.

Mwaka 2014 kampuni ya Facebook iliponunua Whatsapp ilikuwa na watumiaji zaidi ya 500 milioni.

Mwaka Mwaka 2016 programu hiyo ilikuwa na watumiaji Bilioni moja, mambo yakaendelea kubadilika mwaka 2018 ilipofikisha watumiaji bilioni 1.5 duniani kote.

Namba hiyo imezidi kuongezeka kwa kasi ambapo Facebook imetangaza programu hiyo imefikisha watumiaji bilioni mbili tangu kuanza mwaka 2020.

Advertisement