ANTI BETTIE: Hivi ni dhambi kumuoa mtoto wa mama yangu mkubwa?

Sunday July 7 2019

 

Habari anti!

Nina miaka 32, nimetokea kumpenda mtoto wa mama yangu mkubwa. Sina nia ya kumchezea ninataka kumuoa kabisa, tatizo ninaogopa kumuambia kwa sababu ni ndugu yangu.

Nifanyeje?

Sikulaumu kwa kumpenda ndugu yako na kufikia hatua ya kutamani kumuoa, naamini huo ni moyo uliokusukuma kupata tamaa hiyo. Ninailaumu akili yako kwa kushindwa hata kufikiria aibu ambayo utapata ukimueleza dada yako kuwa unataka kumuoa.

Sema na moyo wako, unafahamu vema hicho kitu hakiwezekani kwa mila na tamaduni, bora angekuwa binamu yako.

Halafu ukimwambia anaweza kukuchukia au asiwe huru na wewe kila anapokuona. Tafuta mwanamke mwenye sifa kama za dada yako umuoe, kumueleza wazo lako ni sawa na kumdharau usifanye hivyo utaibua chuki kwenye familia.

Advertisement

Nahisi hawataki kunioa kwa sababu sijasoma

Nina miaka 26, natamani kuolewa lakini sipati wachumba. Anti sina kasoro zaidi ya kutosoma.

Naomba kufahamu ukiwa hujasoma unaweza kukosa mume?

Kutosoma na kuoana au kuolewa havina uhusiano, umri wako pia bado mdogo usiwe na haraka muda ndiyo utakuwa mwamuzi wa haki.

Turudi kwenye suala la kutosoma, kwa nini hujaamua kujisomesha kidogo kidogo kwenye elimu ya watu wazima kama ulikosa elimu rasmi.

Tafadhali ukisoma hapa inuka chukua hatua ili ujiendeleze kielimu , japo ya ufundi hiyo itakusaidia wewe mwenyewe.

Nimechoka mapenzi ya kibubu bubu...

Mke wangu ananinyima raha ya mapenzi kutokana na kung’ang’ania kufanya mapenzi ya kimya kimya.

Kabla ya kuwa naye nilikuwa na wapenzi ambao walikuwa wananivutia kutokana na kuugulia tunapokuwa faragha, nilipomuoa nilijua nitamrekebisha na mambo yataendelea.

Lakini kila nikijitahidi hataki kubadilika, nifanye nini?

Fanya hivi lalamika wewe kadri uwezavyo unapokuwa naye faragha, anza ghafla akikuuliza mwambie unapenda yeye afanye hivyo lakini hataki.

Jambo lingine chukua muda mwingi kumaliza, hilo litamfanya ajiulize kwa nini dozi imebadilika. Akikuuliza hilo nalo mwambie kwa sababu hakuhamasishi.

Ukishindwa hilo kaza moyo, mnapokuwa faragha asipolalamika ahirisha shughuli hiyo, akishangaa mwambie huna hamasa kwa sababu halalamiki.

Fanya mambo hayo mara kadhaa huku ukiongeza kulalamika kuwa hakuhamasishi kabisa kiasi anatishia kupunguza nguvu zako za kiume.

Lalamikia nguvu zako kupungua kutokana na kutohamasishwa, hakuna mwanamke anataka mumewe apungukiwe nguvu za kiume, ataogopa na kuanza malalamiko faragha.

Advertisement