USHAURI WA DAKTARI : Fanya haya ili kujizuia kuwahi kufika kileleni

Mmoja wa wasomaji ameuliza swali ambalo linazungumziwa pia katika mitandao ya kijamii na kwa kuwa linagusa moja kwa moja maisha ya wenza walio katika mahusiano au ndoa nitalijibu kwa faida ya wengine pia.

Nitamnukuu muulizaji, Habari dokta Shita mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 47 nipo katika ndoa kwa muda miaka tisa lakini sasa ndoa yangu iko shakani kutokana na tatizo la kuwahi kufika mshindo.

Najikuta hata dakika moja haiishi tayari nimefika ukingoni, nifanyeje Daktari niweze kuepuka na tatizo hilo.

Jibu: Kuwahi kufika kileleni ni tatizo linalowapata wanaume wengi pasipo kuweka wazi na sababu huwa ni matatizo ya kimwili na kiakili.

Kufika mshindo na kusisimka ni tendo linalohusisha mfumo wa fahamu usio wa hiyari chini ya udhibiti wa ubongo.

Tatizo hili hutokana na mwili wa mwanaume kutiririsha kupita kiasi homoni na kemikali zingine zinazosisimua mwili na kuupa taarifa ubongo ambao hujibu mapigo kwa kutuma ujumbe katika mishipa ya fahamu sehemu za kiume ili kufikia mshindo.

Mwanaume mwenye tatizo hili huwa anafika mshindo chini ya dakika tatu au kama ni mbaya zaidi ni chini ya dakika moja. Kwa kawaida inatakiwa angalau iwe kwa dakika tatu mpaka tano kwa mshindo wa kwanza.

Njia zifuatazo zinaweza kufanyika ili kuweka mwingiliano na mfumo wa fahamu utakaosaidia kuchelewesha kufika mshindo mapema.

Kujijengea kujiamini na kuacha woga mjulishe mwenza wako afahamu kuwa tatizo hili si la kujitakia bali ni la kimwili na kisaikolojia kwa mwanaume.

Kuridhishana si kwa kujamiana pekee bali pia kusisimuana kimwili katika maeneo mbalimbali mwilini kwa muda mrefu.

Mwanaume mwenye tatizo hili anatakiwa kumwandaa mwenza wake kwa muda mwingi zaidi angalau zaidi ya nusu saa katika mzunguko wa kwanza.

Mwenza wa kike anaweza kufanya njia maarufu inaitwa squezing method ambayo wakati mwanaume anapokaribia kufika mshindo ajikatize na kumwacha mwenza wa kike aweke shinikizo kwa kukamua kidogo katika kichwa na shingo ya kiume.

Mwenza wa kike anaweza pia kuweka shinikizo katika daraja la shina la korodani na njia ya haja kubwa, eneo hilo lina tezi dume ambayo ndio inayo kakamaa ili kuweza kufika mshindo kufanya hivyo kunapunguza kasi ya kufika mshindo mapema.

Njia hii imekua ikisaidia sana kwani eneo hilo ndilo lina mshipa wa fahamu unaosisimka na mbinu hii inaweza kufanyika kwa sekunde 30 na kisha kuendelea tena.

Utumiaji wa mpira ya kiume ambayo ni laini isiyo na mafuta mengi au yenye dawa ya ganzi inayosaidia kupunguza msisimko hivyo inaweza kutumika kama njia mojawapo ya kupunguza kufika kileleni mapema.

Njia nyingine ipo ingawa wataalamu wa tiba huwa hawaipendelei ni ile ya kujichua kwa mzunguko wa kwanza kabla ya kuanza na mwenza wako, hofu ya njia ni uwapo wa athari za kimwili na kisaikolojia.

Vile vile mafuta maalum na dawa za kupulizia juu ya ngozi ambazo hutumika kupaka katika kichwa cha uume zinazoupa ganzi hivyo kuchelewesha kupata msisimko na kufikia kileleni.

Unatakiwa kujiamini na kutokuwa mwoga, jione ni mshindi usiyeshindwa. Ongea na wakubwa wenye uzoefu na maisha ya ndoa watakuelimisha zaidi au fika katika huduma za afya kwa ushauri.