Uhusiano kati ya Damu na Tabia

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O. Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota.

Wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea, kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula.

Damu kundi “AB”

Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.

Mazuri yao

Ni rahisi sana kuwa rafiki nao. Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.

Mapungufu yao

Wagumu katika kufanya maamuzi.Wanasahau sana. Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika. Sio waaminifu.Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.Ni watu wabinafsi.

Maisha ya kijamii

Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.

Mahusiano ya mapenzi

Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza.

Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.

Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.

Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha. Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa. Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB. Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga na pia vyakula vitokanavyo na wanyama.