VIDEO: Manara: Simba tumeshtushwa, Wanasimba tulieni

Muktasari:

Ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amezungumzia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ ambapo amewataka wana Simba kuwa watulivu


Dar es Salaam. Ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema taarifa za kutekwa kwa mwekezaji wa timu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ zimewashtua Simba nzima lakini bado wanaamini jeshi la polisi litafanya kazi yake.

Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 11, 2018 Manara amesema taarifa ya Mo kupata matatizo imemshtua kila mmoja na kwamba bado wanaliachia jeshi la polisi kufanya kazi ya kumpata mwekezaji wao.

Amesema kwa sasa Wana-Simba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini Mo Dewji atapatikana akiwa hai.

Amesema wako katika huzuni kubwa kwa kuwa ni jana tu walikuwa naye katika kikao cha bodi ya wadhamini akiwa na furaha wakati wote.