Mawaziri watatu Kenya wahojiwa kutaka kumuua Naibu Rais

Monday June 24 2019

 

Nairobi, Kenya. Mawaziri watatu pamoja na makatibu wakuu watatu kutoka Mkoa wa Kati Kenya wamehojiwa kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua Naibu Rais, William Ruto.

Mawaziri hao walihojiwa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Nairobi.

Waliohojiwa ni pamoja na Joe Mucheru (Teknolojia), Peter Munya (Biashara na Jumuiya ya Afrika Mashariki) na Sicily Kariuki (Afya).

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi, James Macharia ambaye naye ni miongoni mwa mawaziri hao wanaotuhumiwa kuhusika na njama hizo hakutokea katika mahojiano hayo.

Mawaziri hao kwa pamoja walifika katika ofisi za mkurugenzi huyo jana asubuhi baada ya kupokea wito uliotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi katika simu za kiganjani kutoka kwa mmoja wa maafisa wa ofisi ya DCI.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, mawaziri hao waliitwa kwa mahojiano baada ya naibu Rutto kuwasilisha malalamiko yake katika vyombo vya usalama.

Advertisement

Katika malalamiko hayo, Rutto alidai viongozi hao kwa kushirikiana na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali walipanga kumuua walipokutana katika mkutano uliofanyika katika hoteli moja jijini Nairobi.

Kwa upande wa makatibu wakuu waliohojiwa ni pamoja na Andrew Kamau, Joseph Njoroge na Andrew Wakahiu.

Habari zaidi zinasema mawaziri hao walikutana katika Hoteli ya La Mada iliyopo barabara ta Thika jijini Nairobi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kumaliza mahojiano hayo, waziri Munya alisema hakuna mkutano wowote waliowahi kufanywa na mawaziri hao wenye ajenda ya kumuua kiongozi huyo.

Munya alikosoa hatua ya ofisi hiyo kuwaita kwa njia ya simu badala ya kuwatumia barua maalum kw akuwa wao ni viongozi wakuu Serikalini.

“Hili jambo halina ukweli wowote badala yake limepanga kutuchafua majina yetu, tunaomba uchunguzi ukamilike haraka ili taarifa zitolewa,” alisisitiza waziri huyo.

Waziri Munya alisema hata hivyo, malalamiko hayo hayapo kimaanishi na kwamba taarifa pekee iliyopatikana katika ofisi ya DCI inahusu mitandao ya kijamii.

“Tumemueleza kwamba hatujakutana Hoteli ya La Mada kwa ajili ya kupanga njama za kumjua Rutto au mtu mwingine yoyote bali tulikuwa pale kwa sababu sisi ni wanachi wa Kenya na sheria inatulinda kukaa popote,” alisisitiza Waziri Munya.

Waziri hyuo alisema si jambo jema kwa kiongozi huyo kuwatuhumu kwani ina wachafulia majina yao kwa jamii kwa kudhani wao ni waharifu.

Malalamiko hayo yanakuja wakati ambako nchi hiyo inajiandaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2022 baada ya Rais Uhuru Kenyatta kumaliza muda wake.

Advertisement