Chelsea, Tottenham nusu fainali FA

Tuesday March 14 2017

 

London, England. Chelsea na Tottenham wanakutana kwa mara nyingine katika 'derby' ya London kwenye mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la FA, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Wembley.

Fainali nyingine itashuhudiwa Arsenal wakivaana na kikosi cha Pep Guardiola cha Manchester City.

Ushindi wa Chelsea dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Stamford Bridge umetoa matumaini mapya kwa timu hiyo kuimarisha kikosi chake zaidi Ligi Kuu.

Timu hizo zilizokuwa zinapambana  ndizo zilizopo kwenye nafasi sita za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England na Chelsea na Tottenham zitanazokutana kwenye nusu fainali hiyo zikiwa pia kwenye nafasi nne za juu.

Mechi hizo za nusu fainali zimepangwa kufanyika Aprili 22 na 23 siku ambazo ni Jumamosi na Jumapili huku fainali imepangwa kufanyika Jumamosi ya Mei 27.

Arsenal na Tottenham zitakuwa na nafasi nzuri zaidi kutokana na kucheza karibu baada ya kuziondoa Lincoln City na Millwall kila moja.

Manchester City iliiondoa Hudersfield kwa mabao 2-0 na Chelsea ikaiondoa Manchester United kwa bao 1-0 juzi usiku.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho kimepoteza nafasi ya kutetea taji lake la Kombe la FA lakini hata hivyo tayari wametia mfukoni Kombe la Ligi.

Baada ya kutinga nusu fainali, Conte alisema, “ Tulionyesha mchezo mzuri wa kuvutia dhidi ya timu yenye kikosi imara. Wana kikosi kizuri hata kwenye Ligi Kuu.”

Advertisement