Ndanda FC ya Mtwara kusajili wachezaji

Sunday June 19 2016

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Timu ya soka ya Ndanda FC ya Mtwara imepanga kusajili wachezaji saba kwa ajili ya kujiimarisha na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Seleman Kachele amesema :“Sisi tunafuata ripoti ya kocha na katika ripoti hiyo amependekeza kuongezwa kwa wachezaji saba mabao ninaamini kuwa wataongeza nguvu katika timu yetu.Kama kocha atapendekeza lingine, tutamsikiliza kwani yeye ndiyo anajua mapungufu ya kikosi chake yako wapi, ”amesema Kachele.

 

Advertisement