Ngeleja aahidi umeme Sengerema

Monday August 01 2016
Ngeleja

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja

Sengerema.  Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amesema atatenga fedha kutoka kwenye mshahara wake ili zitumike kuweka umeme Kituo cha Afya Kata ya Busisi na Zahanati ya Kijiji cha Mlaga wilayani humo.

Ngeleja ametoa kauli hiyo alipokuwa akihamasisha maendeleo kata za Busisi na Buyagu.

Amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwaondolea kero wananchi kufuata huduma za afya umbali mrefu.

“Nimeamua kufanya hivyo ili niwasaidie wananchi wa jimbo langu hasa wajawazito wanaokwenda kujifungua, ili wapate huduma bora karibu,” amesema Ngeleja.

Advertisement