Rais Magufuli awaapisha Waziri Bashungwa, Kichere na Mhede

Monday June 10 2019

By Elias Msuya, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo Jumatatu Juni 10 amemwapisha  Innocent  Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Joseph Kakunda aliyeenguliwa wiki iliyopita.

Kakunda alienguliwa kufuatia mkutano kati ya Rais Magufuli na wafanyabiashara watano wa kila wilaya nchini uliofanykia Ikulu ya Dar es Salaam wiki iliyopita.

Mbali na Waziri Bashungwa, Rais Magufuli pia amemwapisha Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe baada ya kuondolewa katika nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiiacha nafasi hiyo kwa Edwin Mhede, ambaye pia aliapishwa.

Advertisement