Raza aunga mkono vita dawa za kulevya

Sunday February 19 2017
pic raza

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mohammed Raza.

Dar es Salaam.Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mohammed Raza ameunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya inayoendeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Raza amesema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya vita hiyo ya dawa za kulevya inayoendelea nchini.

“Naunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni imani yangu vita hii dhidi ya dawa za kulevya tutaishinda, kama tulivyomshinda nduli Idd Amini,” amesema Raza.

Aliendelea kwa kusema kuwa, kila Mtanzania anatakiwa kuwa na uchungu na nchi yake kwa kuunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuwa biashara hiyo inadhoofisha nguvu ya Taifa.

 

Advertisement