Russia yapandisha umri wa kustaafu hadi miaka 65

Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Medvedev.

Muktasari:

Nchi hiyo imesema mabadiliko hayo yatafanyika kuanzia mwaka huu hadi 2028 kwa wanaume na 2034 kwa wanawake.

Moscow. Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Medvedev amependekeza kuongeza umri wa wastaafu hadi miaka 65 kwa wanaume na 63 kwa wanawake, ikiwa ni ongezeko kubwa kwa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 90.

 

"Tumependekeza pia muda mrefu wa kufanya mabadiliko hayo, kuanzia mwaka 2019 tunapendekeza kuongeza umri wa kustaafu kwa wanaume kufikia miaka 65 ifikapo mwaka 2028, na miaka 63 kwa wanawake ifikapo mwaka 2034," amesema Medvedev akizungumzia mipango hiyo ambayo itabidi ipitishwe na Bunge.

AFP