TFDA yaburuta 21 mahakamani kwa dawa bandia
Muktasari:
- Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Ofisa Uhusiano wa TFDA kanda ya Ziwa, Martin Malima inaelezakuwa watu hao walinaswa wakati wa zoezi la ukaguzi maalum uliohusisha Maofisa wa TFDA na taasisi zingine za serikali.
Mwanza. Wafanyabiashara 21 wanaomiliki maduka ya dawa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, wamefikishwa mahakamani na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kwa tuhuma za kuuza dawa bandia na zile za serikali kinyume cha sheria.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Ofisa Uhusiano wa TFDA kanda ya Ziwa, Martin Malima inaelezakuwa watu hao walinaswa wakati wa zoezi la ukaguzi maalum uliohusisha Maofisa wa TFDA na taasisi zingine za serikali.
Taarifa hiyo inasema zoezi hilo liliendeshwa kwa kipindi cha miezi sita iliyopita katika Mikoa ya Mara, Simiyu, Geita na Shinyanga.